Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Kituo cha Tafiti za Afrika, kinachohusishwa na Idara ya Masuala ya Fikra na Utamaduni ya Ataba Abbasiyya, kimeanza kutekeleza programu zake za Qur’ani zilizoundwa mahsusi kwa ajili ya wanafunzi na vijana balehe katika Jamhuri ya Nigeria.
Sayyid Muslim al-Jabiri, msimamizi wa Kitengo cha Ulinganiaji wa Kidini katika kituo hicho, amesema kuwa kituo hicho, kwa kushirikiana na Shule ya “Salman Muhammadi” nchini Nigeria, kinatekeleza programu zake kupitia madarasa ya Qur’ani yanayofanyika kwa utaratibu maalumu.
Madarasa hayo yanajumuisha kuhifadhi aya za Qur’ani Tukufu, kufundisha usomaji wa kimatamshi ulio sahihi wa Qur’ani, pamoja na kuwafahamisha wanafunzi kanuni na hukumu za Tajwidi.
Ameongeza kuwa lengo la programu hii ni kuendeleza uwezo wa wanafunzi katika kuhifadhi na kusoma Qur’ani, na kujenga kwa kina uhusiano baina yao na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili kusaidia kuandaa kizazi kitakachokuwa na maarifa sahihi ya Qur’ani.
Shughuli hizi zinafanyika katika mfumo wa programu za kielimu na ulinganiaji za kituo hicho katika baadhi ya jamii za Kiafrika. Programu hizo zinalenga kueneza utamaduni wa Qur’ani, kuunga mkono taasisi za kielimu na kidini, na kuimarisha uwepo wa Qur’ani Tukufu miongoni mwa vizazi vipya.
Maoni yako